USHAWISHI NA UTETEZI KATIKA UKUSANYAJI WA RASILIMALI NA RASILIWATU - PowerPoint PPT Presentation

1 / 12
About This Presentation
Title:

USHAWISHI NA UTETEZI KATIKA UKUSANYAJI WA RASILIMALI NA RASILIWATU

Description:

Ushawishi(Lobbying) na Utetezi (Advocacy) ni dhana zinazotumika pamoja na wanaharakati wengi. Utetezi ni kupigia debe ama kuunga mkono masuala ambayo unayaamini ... – PowerPoint PPT presentation

Number of Views:197
Avg rating:3.0/5.0
Slides: 13
Provided by: africanco
Category:

less

Transcript and Presenter's Notes

Title: USHAWISHI NA UTETEZI KATIKA UKUSANYAJI WA RASILIMALI NA RASILIWATU


1
USHAWISHI NA UTETEZI KATIKA UKUSANYAJI WA
RASILIMALI NA RASILIWATU
  • Imeandaliwa na
  • Alex Mayunga
  • alexmayunga_at_gmail.com
  • Simu 0713 547996

2
Tafsiri
  • Ushawishi(Lobbying) na Utetezi (Advocacy) ni
    dhana zinazotumika pamoja na wanaharakati wengi.
  • Utetezi ni kupigia debe ama kuunga mkono masuala
    ambayo unayaamini
  • Ushawishi ni mchakato unaobuniwa ili kuepika
    mawazo ya wafanya maamuzi ili kupata uungwaji
    mkono wa programu ama mkakati .
  • Maamuzi haya huweza kuwa ya kisera, mkakati,
    sheria ama rasilimali.
  • Ushawishi unalenga kuleta mabadiliko ya kimaslahi
    ama matakwa ya wadau mbalimbali ili yaendane na
    matakwa ya kikundi husika kama vile Asasi,
    Mtandao wa asasi n.k

3
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
  • NGUVU
  • q       Uzoefu wa shughuli za asasi za kiraia
  • q       Uwezo mkubwa unaotokana ushiriki mkubwa
    wa warsha, semina na makongamano mbalimbali.
  • q       Timu ndogo lakini zenye watendaji wa
    kujitolea.
  • q       Mazingira ya kijiografia.
  • q       Kuwa na mtandao mpana wa taarifa na
    shughuli,
  • q       Kuwa karibu na wadau mbalimbali kama
    idara, taasisi za serikali, washirika wa
    maendeleo n.k
  • q       Mtazamo chanya wa wadau juu ya umuhimu wa
    uwepo wa AZISE na Mitandao
  •  

4
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
  • UDHAIFU
  • q       Ukosefu wa Rasilimali
  • Mf. Fedha, vitendea kazi, watendaji
    wenye ujuzi na uzoefu
  • q       Mifumo ya upatikanaji wa Viongozi. Mfano
    Kupigiwa kura ama kuteuliwa bila kuzingatia
    vigezo.
  • q       Kutokuwa na viwango vinavyotambulika vya
    viongozi wa AZISE
  • q       Uchanga wa baadhi ya AZISE
  • q       Kutamani kutumia kila fursa
    inayopatikana.

5
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
  • FURSA
  • Kuwa na mitandao na mashirika mengi yanayofana
    kimalengo na dira.
  • Uwepo wa wadau mbalimbali kama viongozi,
    wafanyabiashara na wadau wa maendeleo .

6
UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
  • VIKWAZO
  • Kukosa uungwaji mkono wa moja kwa moja na wadau
    muhimu.
  • Mtazamo hasi wa jamii juu ya AZISE.
  • Hofu ya utendaji mbovu wa baadhi ya asasi.
  • Ushindani mkubwa wa AZISE/MITANDAO inayofanana.
  • Ukubwa na uwezo wa kirasilimali na rasiliwatu.
  • Hofu ya ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya
    watendaji wa baadhi ya wadau wa maendeleo.
  • Tofauti za shabaha kati ya AZISE na Wadau wa
    Maendeleo.

7
KWA NINI STADI ZA USHAWISHI NI MUHIMU?
  • Kuwa na stadi muhimu za ushawishi kunatuwezesha
    kuweza kuwekeza zadi katika maeneo ambayo tuna
    nguvu, kurekebisha udhaifu wa kiasasi, kutumia
    vizuri fursa zilizopo na kusaka nyingine na
    kikubwa zaidi kuepukana na vikwazo.
  • Kumbuka si kila changamoto katika AZISE /
    Mitandao zinasababishwa na Ufinyu wa Rasilimali
    na Rasiliwatu.

8
MAMBO MUHIMU KATIKA KUKUSANYA RASILIMALI
  • Mingi ya miradi au shughuli ina gharama. Baadhi
    itahitaji kiasi kikubwa cha rasilimali na mengine
    kiasi kidogo cha rasilimali au mikakati kidogo ya
    kukusanya rasilimali.
  • Mambo ya Kuzingatia
  • Makisio ya gharama kwa ajili ya shughuli/mradi.
  • Wadau ambao wanaweza kuchangia wataalamu, vifaa
    au/na pesa.
  • Mpango madhubuti wa kukusanya rasilimali/rasiliwa
    tu katika maeneo yenye upungufu.
  • Mchango wa Washiriki ama watu watakaonufaika na
    mradi/shughuli

9
DONDOO MUHIMU ZA USHAWISHI WA KUKUSANYA
RASILIMALI / RASILIWATU
  • Kabla ya kukutana na mdau wa maendeleo kwa ajili
    ya kuomba rasilimali ni muhimu kujiuliza mawasli
    yafuatayo.
  • Kwa nini tunamfuata mdau A, B na C na sio D?
  • Tunaweza kupata mdau wa kuunga mkono
    wazo/mradi/shughuli yetu?
  • Mdau anajua lolote kuhusiana na asasi/mtandao
    wetu na shughuli zake?
  • Tunajua anajishughulisha na nini, maeneo ya
    kipaumbele, shabaha na malengo yake?
  • Nani ataratibu zoezi la ushawishi inapofikia
    hatua ya kuwasilisha maombi yetu?
  • Mdau anategemea nini toka kwetu?
  • Kitu gani hasa tunataka kuomba?

10
DONDOO MUHIMU ZA KUKUSANYA RASILIMALI
  • 8. Hoja gani tunapaswa kujenga?
  • 9. Tunajua shirika ama watu wa karibu wa mdau
    ambaye wanaweza kumshawishi? Mf. Mbunge, Diwani,
    Meya n.k
  • 10. Kiasi gani cha rasilimali/rasiliwatu
    tunapaswa kuomba? Kiasi maalum ama makisio?
  • 11. Kuna sababu ya kutokuomba kitu chochote cha
    ziada? kama vile mafunzo, vitendea kazi n.k.
  • 12. Tunataka kuambata na kitu chochote
    kinachooneha mafanikio yetu Mfano Ripoti ya
    miradi iliyofanikiwa, Barua za pongezi toks kwa
    wadau wengine, Majina ya walezi ama wajumbe wa
    Bodi ya Udhamini n.k
  •  

11
IPI NI NJIA BORA YA KUKUSANYA RASILIMALIMBINU
YA USHIRIKELI au HOJA?
  • USHIRIKELI
  • Onesha katika mawasilisho yako na jinsi
    unavyowasilisha kwamba unaamini unachokisema na
    umejiridhisha kwamba ni muhimu. Kwa njia hii
    unaweza kumfanya Mdau wa Maendeleo kuvutika na
    kujaribu kuvaa viatu vyako.
  • Kuwa makini usije ukatumia hisia nyingi
    ukaonekana unaomba hisani au kuonewa huruma.
    Unaweza kuonekana mwenye kuhitaji sana, usiye
    mkweli au usiye na utaalamu.
  • HOJA
  • Mbinu hii inakupasa uwe mjengaji mzuri wa hoja
    zenye mashiko kuonesha unajua umuhimu wa mradi
    wako. Usijikite kwenye kutoa ahadi ila onesha
    jinsi gani unaweza kutekeleza mradi/shughuli yako

12
TUNAWEZAJE KUJENGA MAHUSIANO NA ASASI ZENYE
FALSAFA TOFAUTI?
  • Kujenga uhusiano na mashirika ambayo
    tonatofautiana nayo katika falsafa ni jambo jema.
  • Inaongeza sifa kwa asasi, kuongeza uwezekano wa
    mafanikio katika baadhi ya maeneo mnayofanana na
    kuvutia washirika wa maendeleo wapya.
  • Hii huweza kufanikiwa iwapo asasi yenu itafanya
    ushirika kwa kuvutiwa na masuala ya msingi na
    sio haiba za watu.
  • Usiwashambuie watu unatofautiana nao Hoji
    wanayosimamia lakini usiwashambulie.
  • Jadiliana nao kirafiki na jikite zaidi kwenye
    masuala muhuimu.
  • Kinyume chake tatengeneza maadui ambao pengine
    ungeweza kushirikiana nao siku za usoni.
  • Alika watu toka asasi tofauti katika matukio yenu

  • Ahsanteni!
Write a Comment
User Comments (0)
About PowerShow.com