Kundi hili ambalo lilijumuisha wana taaluma mbalimbali tok - PowerPoint PPT Presentation

1 / 29
About This Presentation
Title:

Kundi hili ambalo lilijumuisha wana taaluma mbalimbali tok

Description:

Kundi hili ambalo lilijumuisha wana taaluma mbalimbali toka mikoa na maeneo ... neno Tarafa liondolewe na isomeke 'Kamati za ngazi ya Kata, Kijiji/Mtaa na jamii... – PowerPoint PPT presentation

Number of Views:412
Avg rating:3.0/5.0
Slides: 30
Provided by: euniacem
Category:

less

Transcript and Presenter's Notes

Title: Kundi hili ambalo lilijumuisha wana taaluma mbalimbali tok


1
TAARIFA YA MAJADILIANO SERA YA AFYA
2
UTANGULIZI
  • Kundi hili ambalo lilijumuisha wana taaluma
    mbalimbali toka mikoa na maeneo kadhaa ya utoaji
    huduma yalikuwa na mambo makuu mawili ya kujadili
    ambayo ni
  • Kujadili na kuotoa maoni na maboresho kwenye
    rasimu ya SERA YA AFYA
  • Kujadili mambo yanayohusiana matatizo na
    maboresho ya huduma za Afya zinazotolewa na
    mashirika na asasi za kujitolea ikiwa ni pamoja
    na DDH

3
MAMBO YA AWALI
  • Kikundi kilimchagua Dr. Meshack Massi Mganga Mkuu
    wa Mkoa wa Morogoro kuwa Mwenyekiti, na
  • Bwana Euniace Bandio wa Hospitali ya Taifa
    Muhimbili kuwa Katibu

4
MJADALA KUHUSIANA NA RASIMU YA SERA YA TAIFA YA
AFYA NA MAPENDEKEZO
5
Utangulizi
  • Kikundi kiliona kuwa ilikuwa ni busara kuwa Sera
    ya Taifa ya Afya itayarishwe upya kwa kuwa hii
    iliyopo ambayo ina umri wa zaidi ya miaka kumi,
    imepitwa na wakati kutokana na mabadiliko muhimu
    katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na
    mabadiliko ya kisayansi, kiteknologia, mitindo ya
    maisha na magonjwa

6
Mjadala wa Kifungu hadi kifungu
  • Kikundi kilipitia kifungu hadi kifungu na kufanya
    uhariri na pia mahali pengine kuongeza kifungu au
    kupunguza kinachoonekana umuhimu wake umemezwa na
    kifungu au vifungu vilivyotangulia.
  • Katika majumuisho yetu tutaonyesha sehemu
    zilizopendekezwa kwa marekebisho na
    zinazopendekezwa kwa nyongeza.
  • Zisizoonyeshwa kwenye jumuisho hili inaonyesha
    kuwa kikundi kimekubaliana nayo

7
  • Kikundi kilikubaliana na maelezo mengi ya awali
    ya Sera hii yanayohusu Utangulizi, Hali ya Afya
    na Umuhimu wa Sera
  • Kikundi kinapendekeza kuwa katika kifungu 4.3
    (xiii) uk. wa 9 kisomeke Kuwezesha mabaraza na
    vyama vya kitaaluma kuandaa, kuboresha na
    kusimamia viwango na maadili ya kitaaluma ili
    kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma za Afya na
    Ustawi wa Jamii zilizo bora na salama

8
  • Kuhusiana na Magonjwa ya Mlipuko kifungu 5.2(a)
    uk.10 Maelezo inapendekezwa ifuatavyo
  • Nchi yetu bado inaendelea kukabiliwa na magonjwa
    ya kuambukiza na ya milipuko ya mara kwa mara,
    pamoja na jitihada kubwa za Serikali za
    kukabiliana nayo. Baadhi ya magonjwa hayo
    yameanza kuwa sugu kwa dawa zinazotumika hivi
    sasa na kusababisha ongezeko kubwa la gharama za
    tiba na vifo vingi, mfano Kifua kikuu na Malaria

9
  • Aidha, kuna magonjwa mapya ambayo yameibuka
    duniani na kusambaa kwa kasi, mfano ni ugonjwa wa
    UKIMWI uliosambaa kote hapa nchini. Kuna magonjwa
    mengine yenye sura ya mlipuko ambayo yanaweza
    kuingia nchini, kwa mfano Ebola, Mafua ya Ndege
    n.k., na kutishia afya ya jamii, usalama na
    ustawi wa Taifa, gharama za kuzuia magonjwa hayo
    ni kubwa na zimekuwa zikiongezeka mwaka hadi
    mwaka

10
  • Kifungu 5.4(a) Maelezo Juhudi kubwa zinafanyika
    katika kuboresha
  • Kifungu 5.6(a) Maelezo sentenso ya pili Hii
    imeleta uwiano mzuri wa huduma za afya hapa
    nchini zinazotolewa
  • Kifungu 5.6(c)(i) Serikali itaendelea kuzingatia
    dhana na kuimarisha Afya ya Msingi katika ngazi
    zote ili kuboresha huduma za Afya (Kikundi
    kilipendekeza kuwa Afya ya Msingi iwe namba moja
    (kifungu 5.1)katika eneo hili ndipo mengine
    yafuate)
  • Kifungu 5.10(b) Madhumuni isomeke Kuimarisha
    mfumo na muundo wa utoaji tiba sahihi na salama
    hapa nchini.
  • Kifungu 5.11(c)(iii) Serikali itaimarisha mfumo
    wa matunzo na matengenezo

11
  • Inapendekezwa kuwa kuongezwe kifungu na 5.12
    kitakachozungumzia juu ya Ukusanyaji na Utupaji
    Sahihi Taka zitokanazo na Tiba, kwa pendekezo
    hili basi vifungu vinavyofuatia vinavyoangukia
    kifungu kikuu cha tano (5.0) zitasogezwa mbele
    kwa hesabu kuanzia iliyokuwa 5.12 iwe 5.13 na
    kuendelea hadi iliyokuwa 5.21 iwe 5.22
  • Pendekezo la kifungu cha 5.12 ni kama ifuatavyo

12
  • 5.12 Ukusanyaji na Utupaji salama wa Taka
    zitokanazo na tiba (Medical Waste management)
  • Maelezo yatengenezwe na wataalamu
  • Madhumuni yatengenezwe na wataalamu
  • Tamko la Sera
  • Serikali itaimarisha mfumo wa Utupaji salama wa
    dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi
    vilivyoharibika au kuisha muda wake
  • Serikali na wadau mbalimbali watashirikiana
    katika kuandaa miongozo ya utupaji salama wa taka
    zitokanazo na tiba

13
  • Kifungu 5.14(c)(i) Serikali itaandaa na
    kusimamia kanuni
  • Kifungu 5.15(a) maelezo isomeke kuanzia sentenso
    ya mwisho uk.20 kama ifuatavyo Vile vile,
    kumekuwa na majadiliano ya kutumia chembe hai na
    viini tete katika kuumba binadamu, jambo ambalo
    mataifa hayajakubaliana yaliyobaki yanafutwa na
    kwenda kwenye (b) Madhumuni

14
  • Kifungu 5.8 kuhusu Ubora na Viwango, limejitokeza
    swali kuhusu kuweka tamko kwenye sera kuhusiana
    na ulinganisho wa vifaa tiba (standardization)
    kwa nia ya kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya
    matengenezo (spares) Jambo hili lileta mjadala na
    kuona kuwa kundi kubwa (semina) itoe maoni juu
    yake
  • Hata hivyo kutokana na hali ya sasa ya
    utandawazi, sheria ya manunuzi iliyopo inaonekana
    kupingana na mfumo halisi wa sasa

15
Masuala ya Mtambuka ya Sera
  • Kifungu 6.3(c)(i) Serikali itatayarisha,
    itaboresha na itasimamia mkakati na miongozo ya
  • Katika kujadili maelezo ya kifungu 6.4 kuhusu
    misamaha, ilijitokeza suala la Wazee, kuwa Wazee
    wasio na uwezo wa kifedha wanasamehewa kama
    wengine wote, je kutamka wazee hapo kuna maana
    gani?? Je si kama wengine wote wasio na uwezo, je
    ni vema Wazee wote wasamehewe kama inavyosema kwa
    Watoto, wanawake wajawazito, wenye magonjwa sugu
    n.k

16
  • Katika kulijadili hili kikundi kiliona yafuatayo
  • Kuwa ni kweli kuna wazee wenye uwezo, lakini je
    si nao ni wazee na waliishatumikia nchi kiasi cha
    kutosha
  • Je si kweli kuwa kuna watoto, waja wazito, wenye
    magonjwa sugu wenye uwezo kuliko hata wale
    wasiosamehewa
  • Utekelezaji wake unaonekana kuleta matatizo
    katika watendaji, kwa kuwa wengi wa Wazee wenye
    uwezo ndio wanaijua hii dhana ya msamaha na
    wanadai kusamehewa?
  • Kikundi kinapendekeza semina itoe maoni kuhusu
    hili (Je Wazee wasamehewe kabisa??)

17
  • Kifungu 6.5(c)(v) isomeke Serikali itaweka na
    kusimamia viwango vya majengo
  • Kifungu 6.9(c)(iii) sentenso ya mwisho isomeke
    Aidha Serikali kwa kushirikiana na mabaraza ya
    taaluma na asasi husika.
  • Kifungu 6.15(c)(i) isomeke Serikali itaimarisha
    mkakati wa kuziba
  • Kifungu 6.17(c)(ii) isomeke Serikali itasimamia
    za kusimamia ithibati na mabaraza ya kitaaluma.

18
  • Kifungu 6.18(a) Maelezo inapendekezwa iandikwe
    hivi
  • Mabaraza ya kitaaluma ni vyombo muhimu katika
    kuandaa, kuboresha na kusimamia viwango na
    maadili ya taaluma.Pamoja na kuwepo kwa vyombo
    hivi bado maadili na viwango vya taaluma
    havizingatiwi na baadhi ya wanataaluma.
    Kutokuzingatiwa kunasababisha wananchi kukosa
    huduma bora wanazostahili au kucheleweshwa kupata
    huduma
  • Kifungu cha 6.18(b) Madhumuni nacho kirekebishwe
    kama ifuatavyo
  • Kuwapa wananchi huduma iliyo bora na salama
    inayotolewa na wataalamu wenye kuzingatia viwango
    na maadili ya kitaalamu

19
  • Kifungu cha 6.18(b) Madhumuni nacho kirekebishwe
    kama ifuatavyo
  • Kuwapa wananchi huduma iliyo bora na salama
    inayotolewa na wataalamu wenye kuzingatia viwango
    na maadili ya kitaalamu
  • Inapendekezwa kuwa katika kifungu 6.18(c) Tamko
    la Sera liongezwe tamko moja kama ifuatavyo
  • (iv) Serikali itaendelea kuunda mabaraza ya
    taaluma yatakayoratibu wanataaluma wa sekta ya
    Afya kulingana na mahitaji yatakayokuwepo.

20
  • Kuhusiana na Kifungu namba 7.0 Muundo wa
    Kitaasisi kikundi kinapendekeza marekebisho
    yafuatayo
  • 7.1.2 isomeke Halmashauri za Wilaya, miji,
    manispaa na za jiji badala ya Serikali za mitaa
  • 7.2.1 sentenso ya pili isomeke Aidha itatathmini
    vituo vya kutolea huduma za Afya ili kuhakiki
    ubora huduma zitolewazo

21
  • Kuhusu kifungu namba 8.0 Muundo wa Kisheria
    tunapendekeza
  • Kifungu 8.2 para ya pili neno Tarafa liondolewe
    na isomeke Kamati za ngazi ya Kata, Kijiji/Mtaa
    na jamii
  • Kifungu cha kwanza kinapendekezwa kurekebishwa
    kama ifuatavyo Kutakuwepo na vyombo vya
    kisheria kwa mujibu wa sheria. Mabaraza na bodi
    za kitaaluma za kusimamia taaluma na maadili
    katika utoaji huduma za afya ngazi zote.
    Kutakuwepo na bodi au kamati

22
  • Kifungu 9.0 Mwisho, inapendekezwa isomeke
    HITIMISHO

23
MJADALA KUHUSIANA NA HOSPITALI ZA ASASI ZA
KUJITOLEA NA HOSPITALI TEULE ZA WILAYA
24
MATATIZO
  • Matatizo ya mishahara ya wafanyakazi, hawalipwi
    kwa viwango sahihi
  • Wanatoa misamaha katika hospitali hizi kama
    ilivyo katika zile za Serikali, hata hivyo kuna
    baadhi ya Hospitali hawatoi misamaha kama
    inavyopaswa kuwa.
  • Wafanyakazi wanahama
  • DDH zinapaswa kuingia mikataba na Halmashauri
    badala ya Wizara kama ilivyokuwa zamani
  • Huleta wawakilishi dhaifu katika vikao muhimu

25
  • Halmashauri kutoiona DDH kama hospitali zao
  • Upungufu wa watumishi kwenye Hospitali hizi ni
    kama ilivyo kwenye sekta ya Afya
  • Kutokuwepo na Uwazi katika matumizi ya fedha
  • Tatizo la Secondment linaleta shida udhibiti wa
    watumishi
  • Ajira za Watumishi waliochini ya viwango

26
Matatizo yanaendelea
  • Kutopewa fedha za basket kama zilivyo zile za
    Serikali kwa ngazi za Zahanati na Vituo vya Afya
  • Kuna malalamiko kuwa kwenye Zahanati na Vituo vya
    Afya vya Mashirika haya hawapewi yale yaliyo
    mahitaji yao

27
SERA INASEMAJE
  • Sera inatambua kuwa umuhimu wa utendaji wa vituo
    hivyo, hii ni katika kifungu 6.6 inayohusu
    Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi

28
MKAKATI WA KUONDOA MATATIZO
  • Serikali iendelee kuboresha DDH badala ya kujenga
    Hospitali mpya penye DDH
  • Serikali iendelee kushirikiana na Mashirika ya
    Dini na Hospitali Binafsi kwa kuwa Serikali haina
    uwezo wa kuhudumia wananchi wote
  • Watumishi wa DDH walipwe kwa payrolls
    zilizoandaliwa Wizarani badala ya kuwapelekea
    fedha. Hata hivyo agizo la Serikali la kupitisha
    fedha benki liko palepale

29
MKAKATI unaendelea
  • Kama mishahara ya watumishi itatolewa kama
    ruzuku, basi secondment isiwepo ila ikama zao
    zipitishwe na Wizara kabla ya kuajiri.
  • Kuna umuhimu wa bodi za Afya kuundwa kwa ngazi
    zote na hasa kwa mikoa, na sheria itungwe kuona
    namna ya kusimamia bodi hizi na hasa za mikoa.
Write a Comment
User Comments (0)
About PowerShow.com